Zingatia kuwa:
  1. Malipo utalipia benki au kwa wakala akaunti namba 0150701400100 CRDB ILEMELA ENGLISH MEDIUM SCHOOL.
  2. Unatakiwa kurejesha risit shuleni kwa meneja au Mkurugenzi na si kwa mtu mwingine yeyote.
  3. Ada italipwa kwa awamu tatu kama ifuatavyo hapa chini na hata hivyo unaweza kulipa mara moja au mbili hauzuiliwi.
  4. Haturuhusu mzazi/mlezi kumpatia mtoto pesa kuleta shuleni tafadhali mzazi/mlezi lipa benki au kwa wakala.
Utaratibu wa kulipa karo(ada)
Chekechea
Januari Tsh. 200, 000/=
Julai Tsh. 150, 000/=
Septemba Tsh. 100, 000/=
Jumla Tsh. 450, 000/=
Msingi
Januari Tsh. 350, 000/=
Julai Tsh. 200, 000/=
Septemba Tsh. 50, 000/=
Jumla Tsh. 600, 000/=
Darasa la nne na saba
Januari Tsh. 450, 000/=
Julai Tsh. 200, 000/=
Septemba Tsh. 200, 000/=
Jumla Tsh. 850, 000/=
Huduma zitolewazo shuleni
  1. Huduma ya kwanza
  2. Maji safi na salama ya kunywa wakati wote
  3. Uji/chai na vitafunwa asubuhi wakati wa mapumziko
  4. Chakula cha mchana
Mchanganuo wa ulipaji wa gharama za chakula, shajala (stationery)
Chekechea
Januari Tsh. 200, 000/=
Julai Tsh. 100, 000/=
Septemba Tsh. 20, 000/=
Jumla Tsh. 320, 000/=
Msingi
Januari Tsh. 200, 000/=
Julai Tsh. 100, 000/=
Septemba Tsh. 20, 000/=
Jumla Tsh. 320, 000/=
Darasa la nne na saba
Januari Tsh. 200, 000/=
Julai Tsh. 200, 000/=
Septemba
Jumla Tsh. 400, 000/=
Kumbuka
  1. Wanafunzi wote watalipa chakula cha mchana shuleni, hakuna atakayeruhusiwa kwenda kula nyumbani wala kuletewa chakula kutoka nyumbani.
  2. Mtoto atarudishwa nyumbani iwapo mzazi amechelewa kumlipia mtoto wake na ikiwa hajatoa taarifa yoyote ya kimaandishi na hiyo taarifa ikakubaliwa shuleni.
  3. Mtoto anatakiwa kulipiwa michango ya chakula na shajala siku ya kwanza mara tu anapofika shuleni. Tafadhali fedha hii ilipwe katika ACCOUNT NO. 015071400100 CRDB Bank ILEMELA ENGLISH MEDIUM SCHOOL.
  4. Fedha ya sare (uniform) ni Tsh. 140,000/= ilipwe shuleni siku ya kufungua shule au kabla, ambayo itajumuisha:

    Kaptula au sketi mbili, shati au blauzi mbili, soksi (jozi moja), sweta moja, nguo za michezo (track suit) na tisheti moja zikiwa zimedariziwa nembo ya shule.

    Rim moja (karatasi 500) kwa wanafunzi wote wa madarasa yasiyokuwa na mtihani na rim mbili(karatasi 1000) kwa wanafunzi wa madarasa ya mtihani(darasa la nne na la saba)

    Shajala(stationery) yaani kalamu, penseli, compass, ruler n.k vinapatikana shuleni kwa bei za madukani.
Usafiri unapatikana kwa gharama zifuatazo kwa kila mwezi
Tsh. 50, 000/= (Kanda A)
KILOLENI, NYASAKA, MADUKA TISA, BUZURUGA, NUNDU, MECCO MADUKA TISA, MITI MIREFU, KANGAE, BUZURUGA, NATIONAL
Tsh. 60, 000/= (Kanda B)
MAHINA, MABATINI, MJINI, KIRUMBA, NYAMANORO KONA YA BWIRU, ROCKCITY MALL
Tsh. 70,000/= (Kanda C)
AIRPORT, PASIANSI, MSUMBIJI, KISESA MKUYUNI, IGOMA, NYAMHONGOLO, IGOGO, KISEKE
Tsh. 80,000/= (Kanda D)
IGOMBE, TX, NYEGEZI, CAPRIPOINT ISANGIJO HADI MAKOROSHONI, NYAMWILOLELWA
Kumbuka
  1. Sehemu yote ambaypo haijatajwa hapo juu itatolewa maelezo shuleni kutoka kwa mkurugenzi au menaja.
  2. Mzazi/mlezi atamleta mtoto wake katika kituo maalumu kwa muda ambapo gari litamchukulia na sio kumfuata nyumbani.
  3. Fedha ya usafiri inalipwa kwa meneja au mkurugenzi na inalipwa kabla ya kuanza Huduma.
  4. Huduma ya usafiri itasitishwa siku mbili tu baada ya siku zilizolipiwa kuisha iwapo hakutakuwa na taarifa maalumu shuleni na ikakubalika.
  5. Iwapo gari litafika kituoni lisimkute mtoto, mzazi atalazimika kumleta mtoto shuleni kwa gharama zake.