Mwanafunzi anatakiwa
  1. Mwanafunzi anatakiwa kufika shuleni kabla au saa moja kamili asubuhi na muda wa kutoka shuleni ni saa 11:30 jioni kwa siku zote za masomo.
  2. Kutokuvaa heleni, kupaka wanja, kapaka rangi kucha au kuweka urembo wowote uwe wa kiitikadi, kiimani, kiutamadudi, kishabiki, n.k na kama ni msichana hauruhusiwi kusuka misuko yoyote ile.
  3. Kuvaa sare sahihi za shule siku zote awapo shuleni au nje ya nje ya shule kwenye shughuli za kishule.
  4. Kuheshimu bendera ya taifa na wimbo wa taifa.
  5. Kuheshimu watu rika zote.
  6. Kujiepusha na tabia zote mbaya kama vile lugha chafu, ugomvi n.k
  7. Kutokumiliki vitu vya thammani kama vile fedha, simu, flash, n.k awapo shuleni.
Mzazi/Mlezi anatakiwa
  1. Kumlipia mtoto wake ada kamili na michango yote kikamilifu na kwa muda muafaka ili kuepika usumbufu
  2. Kuhudhuria vikao vyote vitapoitishwa na uongozi wa shule ili kuboresha maendeleo ya mwanafunzi.
  3. Kuvaa mavazi ya staha na kujiepusha na lugha chafu awapo shuleni kwa shughuli yoyote.
Apply Now